Posts

Showing posts from 2018

SARATANI YA MATITI

UTANGULIZI Tunaishi kwenye ulimwengu ambao una magonjwa mbali mbali ya saratani, lakini saratani ya matiti inaongoza kwa kuathiri wanawake wengi zaidi kwa sasa. Visababishi (causes) vya saratani havijajulika bado hivyo tafiti zinaendelea ili kubaini. Je saratani ya matiti ni ugonjwa gani? Dalili zake ni zipi? Imeathiri kiasi gani cha watu kwa miaka ya hivi karibuni? Jinsi gani ya kujikinga na saratani ya matiti?, je kuna tiba ya saratani ya matiti? Inaweza kuwapata wanaume pia? je kuna namna ya kujichunguza kubaini kama una saratani ya matiti? SARATANI YA MATITI Saratani ya ni matokeo ya mgawanyiko usio wa kawaida wa seli (cell) za mwili (matiti/titi) ambao huchangiwa na mabadiriko ya vinasaba (DNA) kisha seli zisizokua za kawaida huzalishwa, seli mpya za saratani zilizozalishwa huweza kuathiri seli zingnine (healthy cell) hivyo ugonjwa kusambaa au kujirundika sehemu moja. je wanaume pia wanaweza kupata saratani ya matiti? • Jibu ni ndiyo, pia mwaume anaweza kupata saratani ya...

Usiruhusu Watu Watembee Kwenye kichwa chako!!

Huwenda upo kwenye wakati mgumu, au ulishapitia kipindi kigumu sana katika Maisha yako, na yote hayo kuna watu wameyasababisha na ukahisi una kila sababu ya kuwachukia watu hao. Nikuambie rafiki, hutakiwi kumchukia mtu yeyote kama Kweli uko makini na Maisha yako. Hata Kama Alitaka kukuuwa akakukosa, bado huna sababu ya kumchukia. Hii nikwasabu, unapomchukia mtu unamruhusu atembee kwenye akili yako muda wote.na huo ni uamuzi mbaya kabisa, kumbuka akili yako ina uwezo mkubwa Sana Mungu aliyouweka ndani yako.Unapowaruhusu watu watembee kwenye akili yako wanaharibu huu uwezo mkubwa uliyondani yako.uwezo wenye nguvu ya ajabu ya kuhamisha milima. Napia unajiweka dhaifu unapomchukia mtu.ni Sawa nakumbeba halafu huna unakompeleka,jitue basi huo mzigo ili uwe huru. Hebu Jaribu kuangalia Vitu mwanadam alivyogundua na kutengeneza, ukiangalia ndege, Meli, Majengo marefu kabisa nk, vyote vilianzia kwenye akili iliyotulizana,then vikawa umbo halisi.Usifanye Kosa kuruhusu watu waharibu uwezo Huu ...

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

Image
Kitu ambacho b,dam anapigania sana katika Maisha yake ni kuwa na Maisha yaliyo nafuraha.kila mtu Anapenda kuwa na furaha katika Maisha yake. Tunatafuta kazi, tunatafuta watoto na tunafanya mengi ila tukiamini yatatimiza hitajio la moyo wetu nakutuletea furaha.Baada yakujua kwamba tunahitaji furaha, shida inakuja kwamba tunaipataje iyo furaha ya Kweli? Ndipo hapo tunapofanya Vitu mbali mbali tukiamini vitatuletea furaha. Na ile furaha tunayotarajia mwisho wa sku hatuipati kwakuwa hatufuati ile misingi sahihi ambayo ndio hutupelekea kuwa na furaha katika Maisha yetu. Ndipo mwandishi Wa kitabu, The book of happiness, by Heather Summers & Anne Watson walivyoamua kutuweka wazi juu ya mambo mbali mbali kuhusu furaha. Haya Hapa ni machache katika niliyojifunza katika kitabu hiki.  1 .Mazingira yanayotuzunguka ni moja ya Vitu ambavyo vinaweza kutupa furaha au kutunyima furaha. Ni hivi, Kama unaishi kwenye nyumba ambayo huipendi, unaishi maeneo ambayo huyapendi,unafanya kazi ambayo...

Tafakuri ya Maisha.

Kuna wakati katika Maisha unaweza hisi kwamba wewe ndio mwenye matatizo makubwa kuliko watu wote duniani.mpaka unafikia hatua yakujiuliza maswali magumu kwamba Kwanini wewe tu siku zote? Mbona matatizo hayaishi likitoka hili linakuja hili? Nikuambie rafiki yangu,wala huna matatizo makubwa kiasi hicho,tatizo letu kubwa ni kwamba tunaangalia zaidi matatizo yetu kuliko Neema tulizopewa. Na hii nikwasababu tunahisi labda tunastahili zaidi kuwa nazo ndio maana hatuzipi umuhimu wake. Labda umetafuta ajira Kwa muda mrefu bila mafanikio, hilo bado si tatizo kubwa kwako,hivi Unajua kuna Mtu hana miguu Wala mikono lakini bado anafurahia Maisha yake! Kwakuwa anaaamini ana sababu nyingi zakufurahi kuliko kuhuzunika. Wakati wewe unafikiri una matatizo makubwa kwakuwa unaumwa wiki ya Pili sasa. Kuna mwingine kalala kitandani mwaka mzima sasa na hajui mustakabali Wa afya yake. Kuna mwingine Kaambiwa atatumia dawa Maisha yake yote kutokana na maradhi yakudumu aliyo nayo. Kama una miguu na mikono ...

MAISHA

Kuna wakati katika Maisha unapitia mambo  magumu sana, na kila ukijaribu kuondokana na hali hiyo bado hupati majibu sahihi. Nikuambie rafiki, huo ndio wakati unatakiwa kuishi hali hiyo Kwa MUDA!huwa tunasahau kuwa MUDA nao ni tiba ya matatizo yetu.Yape matatizo yako MUDA. kama vile unavyoweza kuipenda nyumba ilihali imefungwa na hujui kilichopo ndani, basi yapende matatizo yako uliyoshindwa kuyatatua. Kuna watu wanapenda nyimbo japo zimeimbwa Kwa Lugha wasioifahamu,kwanini usiipende Hali uliyonayo Kwa MUDa? Kumbuka kila Hali unayopitia Mungu anamakusudi juu yako,huwenda hata matatizo yako yakiondoka sasa hutaweza kuyafurahia Maisha Au hutaweza kuishi katika Hali hiyo tulivu yakukosa changamoto. Nikutakie siku mpya yakuyaendea mafanikio rafiki yangu. Elishad bashir Irshady12@gmail.com. Karibu tujifunze zaidi kwenye amkanauishi.blogspot.com.

FIKRA PEVU.

Usikubali Maisha yako yategemee Vitu hivi:- 1.Pesa.    Mtu maskini kuliko wote duniani ni Yule     ambaye alicho nacho katika Maisha    yake ni pesa tu.niukweli uliowazi kuwa pesa inasaidia upate mahitaji yako ya msingi, uweze kuwasaidia watu wako, uweze kuishi Maisha unayotaka.lakini kama pesa itakuwa ndio sabab yako kuu ya kuishi, basi umechagua Maisha mabaya. Tafuta pesa na miliki kiasi unachohitajii, ila usiache kutengeneza maeneo mengine ya Maisha yako. >Usisahau kuwa bora katika mahusiano yako na watu wengine, >Usitegemee pesa iwe chanzo cha furaha kwako, jitahid kutengeneza furaha kutoka ndan yako. 2.Mahusiano. "The worst loneliness is not to be comfortable with yourself"Mark Twain. Ni kitu kibaya sana kama huwez kuwa na furaha kwakuwa  mwenyewe katika Maisha. Furaha yako itakapotegemea Uwepo Wa mtu fulani,ilihali sote tunajua kuwa katika yaliyo nje ya uwezo wetu ni maamuz ya watu wengine,basi umechagua Maisha mabaya kuishi....

FIKRA PEVU

Huwezi timiza malengo makubwa uliyojiwekea, Kama hujawa tayari kupambana na changamoto na vikwazo Kwa muda mrefu. Katika Maisha kila Mtu anataman kuwa na Maisha Mazuri,maisha ambayo yamejitosheleza. Lakini kutamani peke yake hakujawahi kufanya kitu kiwe kama hujachukua hatua,na pale unapochukua hatua pia mambo hayawi rahisi vile vile. Utakutana na kila la kukukatisha tamaa akiwepo wewe mwenyewe, utajiambia Haya yote Yanini? Kwanini nisifanye mambo mengine?. Rafiki, Maisha hayana tabia yakuruhusu upate unachotaka Kwa wepesi,mpaka uwe tayari kupoteza baadhi ya Vitu, uwe tayar kupambana na kila jiwe Maisha yatalokurushia. Nipale tu utakapo kuwa king'ang'anizi, ndipo Maisha yatakuwacha upate unachotaka na ufanye unachotaka. Nikutakie sku njema, katika kupambana ili ufikie ndoto yako. Elishad Bashir. Irshady12@gmail.com.

"NAUZA FIGO"

                         "NAUZA FIGO" Habari rafiki, Hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kutujalia mikononi mwetu siku nyingine mpya kabisa. Binadamu mwanzoni kabla yakugundulika pesa alikuwa na mfumo flani wakumuwezesha kupata kile ambacho hana,ambao ilikuwa nikubadilishana vitu,mfugaji akihitaji mahindi anampa mkulima ng'ombe naye anapewa mahindi(Barter trade).ilikuwa na ugumu wake kwasababu mpaka umpate mtu mwenye shida ya ng'ombe ili yeye akupe mahindi,unaweza zunguka na ng'ombe kwa mda mrefu bila mafanikio. Baadae ikagundulika pesa,ikawa imerahisisha sana kiasi kwamba ukishakuwa na pesa unakuwa na huru wa kununua chochote unachohitaji. Changamoto inakuja sasa kwenye utafutaji wa hii pesa.kutafuta pesa yakula tu haijawa tatizo sana,tatizo nikwamba mahitaji yetu hayaishii kwenye kula.kila mtu anahitaji kuwa na mafanikio makubwa kwenye fedha.Na mafanikio haya ...

ISHUKURU SANA JANA YAKO

"Use the lessons you have learned from your past to rise to a whole new level of awareness and enlightenments"Robin Sharma. Habari rafiki!kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Yule aliyetuwezesha kuiona siku hii mpya ambaye ni Mwenyez Mungu Muumba mbingu na ardhi.Hatuna budi pia kuitumia siku hii kuongeza thaman katika Maisha yetu,kwani ni wengi walitamani wawepo ila hawapo. Karibu sana rafiki.hakika Jana yetu imetawaliwa na mambo Mengi yakiwemo mabonde na milima, makosa na Maudhi pamoja na usaliti mbali mbali lakini yalishapita na Leo tuko katika wakati Wa sasa.Jana yetu ina nafasi kubwa ya kujenga au kuharibu maisha yetu ya sasa.Pale utakapoanza kujilaumu Kwa makosa ambayo uliyafanya na kukupa matokeo mabaya na kukupa wakati mgumu,pale utakapoanza kuwalaumu watu Kwa Yale waliokufanyia mabaya na kujipa sababu kuwa wao wamekuharibia maisha,basi umeamua kupoteze nguvu na muda wako wa sasa kwenye wakati uliopita.Na huo ni uamuzi mbaya Sana katika Maisha yako.Uamuzi sahihi ni ...

Mambo niliyojifunza katika kitabu cha THE COMPOUND EFFECT cha mwandishi DARREN HARDY.

Habari ndugu msomaji wa makala hii! karibu tuendelee kujifunza ili kuweza kwenda sawa na maish . a ya sasa yasiokwisha changamoto. As long as you live,keep learning how to live-Lucius Annaeus Senneca.Mwanafalsafa huyu anatuambia"kwakuwa tunaishi,basi hatuna budi kujifunza namna ya kuishi" Maisha uliyonayo sasa ni matokeo ya mambo mbalimbali madogo madogo uliyoyafanya huko nyuma,maisha   yoyote yale uliyo nayo kwa sasa,ikiwa ni mazuri   au mbaya,bas jua ni matokeo. Twende moja kwa moja   rafiki tukaangazie yale niliyojifunza kwenye kitabu tajwa hapo juu;   Hatua ndogo na makini unazochukua katika maisha yako zinakupelekea katika mafanikio makubwa.Ni ukweli usiopingika kuwa mafanikio ni matokeo,sasa ili upate matokeo mazuri kuna mambo mengi unayotakiwa kuyafanya ili uweze kupata matokeo hayo,na mambo hayo wala si makubwa sana ,bali yanafanywa kwa muda mrefu mno mpaka yanakuwa utamaduni au tabia na mwisho huleta matokeo makubwa.   Kufanya kazi...

TATIZO SIO KIFO, TATIZO NI KILE KINACHOKUFA NDAN YETU TUNGALI HAI.

Habar ndugu msomaj wa makala hii!,karibu tuendelee kujifunza ili kuweza kwenda Sawa na Maisha yasasa yasiokwisha changamoto. Binadam tofaut na viumbe wengine, kuna uweze mkubwa Sana uko ndan yetu.Uthibitisho wa hilo upo hasa kwenye Mazingira yanayotuzunguka, unapojaribu kutazama Vitu Kwa jicho la fikra, Utagundua Vitu vya ajabu Sana binadam kafanya.vitu hivyo vimeongeza thaman kubwa katika Dunia na Maisha yamekuwa bora sana siku hadi siku.Sasa hivi Unaweza Amka asubuh ukamsalimia mama yako kijijini au ndgu yako ambaye Yuko Marekani ilihali uko bado kitandan Kwa njia ya simu tu either call, Whatsup au hata SMS yakawaida. Kwa kutazama Kawaida Unaweza ona hili ni jambo la Kawaida tu kwakuwa umeshalizoea, ila Kwa Hakika ni kazi kubwa Sana imefanywa mpaka wewe unafurahia Maisha ivyo.watu wamekesha, wamelala njaa mpaka wakagundua simu Kama njia ya mawasiliano. Ukitembea mjini utaona majengo marefu kupita Kias huwez amini kuwa bi/dam Ndo kajenga. Ndege zinatembea angani, meli zenye mizigo y...