SARATANI YA MATITI
UTANGULIZI Tunaishi kwenye ulimwengu ambao una magonjwa mbali mbali ya saratani, lakini saratani ya matiti inaongoza kwa kuathiri wanawake wengi zaidi kwa sasa. Visababishi (causes) vya saratani havijajulika bado hivyo tafiti zinaendelea ili kubaini. Je saratani ya matiti ni ugonjwa gani? Dalili zake ni zipi? Imeathiri kiasi gani cha watu kwa miaka ya hivi karibuni? Jinsi gani ya kujikinga na saratani ya matiti?, je kuna tiba ya saratani ya matiti? Inaweza kuwapata wanaume pia? je kuna namna ya kujichunguza kubaini kama una saratani ya matiti? SARATANI YA MATITI Saratani ya ni matokeo ya mgawanyiko usio wa kawaida wa seli (cell) za mwili (matiti/titi) ambao huchangiwa na mabadiriko ya vinasaba (DNA) kisha seli zisizokua za kawaida huzalishwa, seli mpya za saratani zilizozalishwa huweza kuathiri seli zingnine (healthy cell) hivyo ugonjwa kusambaa au kujirundika sehemu moja. je wanaume pia wanaweza kupata saratani ya matiti? • Jibu ni ndiyo, pia mwaume anaweza kupata saratani ya...