Posts

Showing posts from July 29, 2018

Usiruhusu Watu Watembee Kwenye kichwa chako!!

Huwenda upo kwenye wakati mgumu, au ulishapitia kipindi kigumu sana katika Maisha yako, na yote hayo kuna watu wameyasababisha na ukahisi una kila sababu ya kuwachukia watu hao. Nikuambie rafiki, hutakiwi kumchukia mtu yeyote kama Kweli uko makini na Maisha yako. Hata Kama Alitaka kukuuwa akakukosa, bado huna sababu ya kumchukia. Hii nikwasabu, unapomchukia mtu unamruhusu atembee kwenye akili yako muda wote.na huo ni uamuzi mbaya kabisa, kumbuka akili yako ina uwezo mkubwa Sana Mungu aliyouweka ndani yako.Unapowaruhusu watu watembee kwenye akili yako wanaharibu huu uwezo mkubwa uliyondani yako.uwezo wenye nguvu ya ajabu ya kuhamisha milima. Napia unajiweka dhaifu unapomchukia mtu.ni Sawa nakumbeba halafu huna unakompeleka,jitue basi huo mzigo ili uwe huru. Hebu Jaribu kuangalia Vitu mwanadam alivyogundua na kutengeneza, ukiangalia ndege, Meli, Majengo marefu kabisa nk, vyote vilianzia kwenye akili iliyotulizana,then vikawa umbo halisi.Usifanye Kosa kuruhusu watu waharibu uwezo Huu ...