MAMBO NILIYOJIFUNZA KATIKA KITABU CHA BLESSED IN DARK PLACES.BY Joel Osteen.
katika maisha watu huwa kuna wakati wanapitia vipindi vigumu.Katika vipindi vigumu ndio wakati ambao mtu huhisi kwamba dunia haimtaki tena na Mungu pia amemsahau.Pia wakati huu ndio wakati ambao mtu huhisi kwamba yeye ndo basi tena,na hawezi tena kurudi katika maisha yake ya mwanzo. Ila ukweli hauko hivyo,kwani ni katika vipindi vigumu ndipo hutokea washindi.Watu wengi waliofanikiwa katika jambo fulani,ukifuatilia utakuta kuwa walipitishwa kwanza kwenye wakati mgumu ndio yakapatikana matokeo ambayo wengi tunayaona.Mara nyingi tunaangalia matokeo ndio maana tunahisi fulani ana bahati na wewe huna,lakini nyuma ya bahati kuna mchakato amepitia. Mwandishi Joel Osteen ameelezea mambo makubwa sana katika kitabu chake cha Blessed in the Dark Places.Haya hapa ni baadhi tu ya mambo niliyojifunza kwenye kitabu hicho kutoka ukurasa wa 1-45. 1 .Usilalamike sana unapopitia wakati mgumu kwenye maisha yako,huo wakati mgumu ndio Mungu huutumia kupitisha neema zake kwako. Kwenye wakati huu ...