"NAUZA FIGO"
"NAUZA FIGO" Habari rafiki, Hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kutujalia mikononi mwetu siku nyingine mpya kabisa. Binadamu mwanzoni kabla yakugundulika pesa alikuwa na mfumo flani wakumuwezesha kupata kile ambacho hana,ambao ilikuwa nikubadilishana vitu,mfugaji akihitaji mahindi anampa mkulima ng'ombe naye anapewa mahindi(Barter trade).ilikuwa na ugumu wake kwasababu mpaka umpate mtu mwenye shida ya ng'ombe ili yeye akupe mahindi,unaweza zunguka na ng'ombe kwa mda mrefu bila mafanikio. Baadae ikagundulika pesa,ikawa imerahisisha sana kiasi kwamba ukishakuwa na pesa unakuwa na huru wa kununua chochote unachohitaji. Changamoto inakuja sasa kwenye utafutaji wa hii pesa.kutafuta pesa yakula tu haijawa tatizo sana,tatizo nikwamba mahitaji yetu hayaishii kwenye kula.kila mtu anahitaji kuwa na mafanikio makubwa kwenye fedha.Na mafanikio haya ...