"NAUZA FIGO"
"NAUZA FIGO"
Habari rafiki,
Hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kutujalia mikononi mwetu siku nyingine mpya kabisa.
Habari rafiki,
Hatuna budi kumshukuru Muumba kwa kutujalia mikononi mwetu siku nyingine mpya kabisa.
Binadamu mwanzoni kabla yakugundulika pesa alikuwa na mfumo flani wakumuwezesha kupata kile ambacho hana,ambao ilikuwa nikubadilishana vitu,mfugaji akihitaji mahindi anampa mkulima ng'ombe naye anapewa mahindi(Barter trade).ilikuwa na ugumu wake kwasababu mpaka umpate mtu mwenye shida ya ng'ombe ili yeye akupe mahindi,unaweza zunguka na ng'ombe kwa mda mrefu bila mafanikio.
Baadae ikagundulika pesa,ikawa imerahisisha sana kiasi kwamba ukishakuwa na pesa unakuwa na huru wa kununua chochote unachohitaji.
Changamoto inakuja sasa kwenye utafutaji wa hii pesa.kutafuta pesa yakula tu haijawa tatizo sana,tatizo nikwamba mahitaji yetu hayaishii kwenye kula.kila mtu anahitaji kuwa na mafanikio makubwa kwenye fedha.Na mafanikio haya yana misingi ambayo kwetu imekuwa migumu.Ugumu huu unawafanya watu watafute njia za mkato zakuwa na mafanikio yakiuchumi.Ambazo njia hizi mara nyingi hazina matokeo mazuri,na wala hazileti yale mafanikio yakudumu yaliyotarajiwa.
Kutokana na kukua kwa teknologia yakiutabibu hapa nchini kwetu,Tuliskia kwenye vyombo vya habari kuwa zoezi la kupandikiza figo linafanywa sasa ivi hapa nchini.na kuna watu au mtu tayari alishafanyiwa zoezi hilo na akapona.
Taarifa niliyokutana nayo juzi,ni ya watu kutangaza kuwa wanauza figo zao.Japo walikuja wakajibiwa kuwa figo haziuzwi,bali hutolewa katika mazingira yakiundugu na kijamii,na si biashara.sasa ni jambo lakushangaza kidgo lakini huishii kwenye kushangaa tu,kipo kitu kikubwa sana cha kujifunza.Na hapa kikubwa cha kujifunza nikwamba watu wanataka kuwa matajiri lakini hawatak kufanya kazi,yaani wanakwepa ile misingi na kanuni zakuwa na mafanikio kifedha.
Mtu anaamini akishauza figo atapata pesa nyingi atakuwa anakula tu.wala hafikirii madhara ambayo anaweza kuyapata kwa kufanyiwa zoez hilo.Na pia ukweli nikwamba hiyo fedha hata akiipata haiwezi kumsaidia kitu maana iko nje yakiwango chake cha fedha alichonacho kichwani mwake.kwaiyo kupata fedha kama hizo nikujiongezea matatizo mengine makubwa.kuwa na pesa nyingi kwa mkupuo, nikubaya kuliko kutokuwa na pesa kabisa.
Mafanikio ya kifedha kama mafanikio mengine yoyote yana misingi na kanuni zake,na moja ya msingi mkubwa ni KUFANYA KAZI TENA KWA BIDII SANA.
Sasa bi/dam huwa hatupendi kujisumbua sana na wala hatuna subira.kukosekana kwa subira kunatufanya tutake mafanikio ya haraka.
Sasa bi/dam huwa hatupendi kujisumbua sana na wala hatuna subira.kukosekana kwa subira kunatufanya tutake mafanikio ya haraka.
Ndio maana wenzetu wanauza figo zao,wengine wanashinda na kukesha wakicheza bahati nasibu(biko,tatu mzuka,moja special nk)wakiamini watashinda nakuwa matajiri mara moja.Unaweza kusema kwani sinikweli wanashinda?
Nikweli wanashinda,ila nikuambie hata ikatokea ukashinda,kuyapata mafanikio itakuhitaji muda na elim zaid.
Ndio maana hata wanaoshinda pesa nyingi tunashuhudia hawafanyi chochote.
Wanaishia kurudi katika maisha yao yakawaida baada ya pesa kuwaishia.
Nikweli wanashinda,ila nikuambie hata ikatokea ukashinda,kuyapata mafanikio itakuhitaji muda na elim zaid.
Ndio maana hata wanaoshinda pesa nyingi tunashuhudia hawafanyi chochote.
Wanaishia kurudi katika maisha yao yakawaida baada ya pesa kuwaishia.
Nikutakie kila la kheri katka safari yako ya mafanikio.
Elishad Badhiru.
Irshady12@gmail.com
Karibu na ututtembelee
Katika mtandao wetu wa
Irshady12@gmail.com
Karibu na ututtembelee
Katika mtandao wetu wa
AMKA NA UISHI.
Comments