FIKRA PEVU.

Usikubali Maisha yako yategemee Vitu hivi:-
1.Pesa.
   Mtu maskini kuliko wote duniani ni Yule 
   ambaye alicho nacho katika Maisha
   yake ni pesa tu.niukweli uliowazi kuwa pesa inasaidia upate mahitaji yako ya msingi, uweze kuwasaidia watu wako, uweze kuishi Maisha unayotaka.lakini kama pesa itakuwa ndio sabab yako kuu ya kuishi, basi umechagua Maisha mabaya.
Tafuta pesa na miliki kiasi unachohitajii, ila usiache kutengeneza maeneo mengine ya Maisha yako.
>Usisahau kuwa bora katika mahusiano yako na watu wengine,
>Usitegemee pesa iwe chanzo cha furaha kwako, jitahid kutengeneza furaha kutoka ndan yako.

2.Mahusiano.
"The worst loneliness is not to be comfortable with yourself"Mark Twain.
Ni kitu kibaya sana kama huwez kuwa na furaha kwakuwa  mwenyewe katika Maisha. Furaha yako itakapotegemea Uwepo Wa mtu fulani,ilihali sote tunajua kuwa katika yaliyo nje ya uwezo wetu ni maamuz ya watu wengine,basi umechagua Maisha mabaya kuishi.kwasabab maamuzi ya huyo mtu huyamiliki wewe, any time Atasema uhusiano wenu uishie hapo,je utaishi?
Mahusiano ni kitu kizuri,na hakuna anayebisha katika ilo.
Ila kuamini kuwa huwezi kuishi bila ya mtu fulani, ni uongo mkubwa uliopitiliza.kitu pekee ambacho hupaswi kukikosa kwenye maisha yako ni pumzi peke yake. Vingine vyote unaweza kuvikosa na ukaishi Maisha mazuri kabisa yenye utimilifu.

3.Maoni ya watu wengine.
Tuko katika kipind ambacho watu wanapenda sana kutoa maoni juu ya kila kitu.lakini Maisha mabaya kabisa ni pale utakapoamua kuishi Maisha ya kuwaridhisha watu wengine.
Na pia Kama umeshakuwa mtu mzima, basi Hakikisha kila unachofanya kinatokana na maamuzi yako wewe mwenyewe,hii ni kwasabab, madhara Yoyote yatakayojitokeza wakuyabeba niwewe na si mtu mwingine.
Na kitu cha muhim kabla hujafanya kitu chochote, kwanza jiulize Hicho unachofanya Kina umuhim katika Maisha yako?

4.belief limit(ukomo wa imani yako)
Wakati mwingine unakuwa mwepesi kuamini kuwa mambo hayawezekani. Ila kiuhalisia kila kitu unachoamini hakiwezekani basi kinawezekana.

Ni imani yangu umejifunza kitu katka mambo haya. Yazingatie, Hakika hayatakuacha kama ulivyokuwa kama utaamua kuyaweka katika matendo.

Elishad bashir
Irshady12@gmail.com.
Karibu tujifunze kwenye
amkanauishi.blogspot.com.

Comments

Popular posts from this blog

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

SARATANI YA MATITI