SARATANI YA MATITI
UTANGULIZI
Tunaishi kwenye ulimwengu ambao una magonjwa mbali mbali ya saratani, lakini saratani ya matiti inaongoza kwa kuathiri wanawake wengi zaidi kwa sasa. Visababishi (causes) vya saratani havijajulika bado hivyo tafiti zinaendelea ili kubaini.
Je saratani ya matiti ni ugonjwa gani? Dalili zake ni zipi? Imeathiri kiasi gani cha watu kwa miaka ya hivi karibuni? Jinsi gani ya kujikinga na saratani ya matiti?, je kuna tiba ya saratani ya matiti? Inaweza kuwapata wanaume pia? je kuna namna ya kujichunguza kubaini kama una saratani ya matiti?
SARATANI YA MATITI
Saratani ya ni matokeo ya mgawanyiko usio wa kawaida wa seli (cell) za mwili (matiti/titi) ambao huchangiwa na mabadiriko ya vinasaba (DNA) kisha seli zisizokua za kawaida huzalishwa, seli mpya za saratani zilizozalishwa huweza kuathiri seli zingnine (healthy cell) hivyo ugonjwa kusambaa au kujirundika sehemu moja.
je wanaume pia wanaweza kupata saratani ya matiti?
• Jibu ni ndiyo, pia mwaume anaweza kupata saratani ya matiti (male breast cancer) japo bado saratani hii sio maarufu sana kwa wanaume.
(Hivyo hapa tutajadili kuhusu saratani ya matiti kwa wanawke)
Kwamujibu wa ripoti ya Shirika la afya duniani (WHO), inakadiriwa kua wanawake zaidi ya milioni 1.5 wanapata saratani hii kila mwaka, pia ripoti ya mwaka 2015 inaonesha kutokea kwa vifo vya wanawake zaidi ya 570,000 kutokana na Saratani ya matiti.
DALILI ZA SARATANI YA MATITI
Dalili kuu ya tatizo hili ni uwepo wa uvimbe ndani ya matiti/titi ambao hata mwanamke akijitomasa anaweza kuuhisi, maumivu au kutokua na maumivu yoyote kwenye uvimbe huo pia uvumbe huu huweza kukaa au kusambaa hadi kwenye kwapa la mkono.
Dalili zingine ni:-
• Kutokwa na usaha/damu/uchafu kwenye chuchu za matiti/titi
• Uvimbe kwenye kwapa
• Kubonyea/kupinduka kwa chuchu (kama inavyooneka kwenye picha)
• Kubadilika kwa umbo la matiti/titi
• Maumivu ya matiti/titi au kwapa ambayo ni endelevu hata baada ya kuisha kwa mzunguko wa hedhi. ( lakini maumivu si dalili kuu ya moja kwa moja kuhisi tatizo hili)
NB: Uwepo wa uvimbe kwenye matiti/titi haina maana ya moja kwa moja kwamba ni saratani ya matiti, hivyo baada ya kuona hizo dalili ni vyema kwenda hospitali kufanya uchunguzi/vipimo zaidi kubaini tatizo.
VICHOCHEO VINAVYOWEZA KUPELEKEA KUPATA SARATANI YA MATITI (Risk factors)
Ndugu msomaji, kumbuka kwamba visababishi vya ugonjwa huu bado havijulikani, lakini kuna vichocheo au mazingira hatarishi ambayo yanaweza kuchochea kupata saratani hii ya matiti (risk factors). Navyo ni:
• Maumbile (genetics), 5% mpaka 10% ya wanawake hurithi saratani hii kutoka kwenye uzao wao. Hivyo ina maana kwamba saratani inaweza kupita kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine.
• Mfumo mbovu wa maisha (life style), tabia kama vile unywaji wa pombe kupindukia, uvutaji wa sigara. Tabia hizi zinaweza kuchochea mtu kupata saratani ya matiti au aina zingine za saratani.
• Kama umewahi kuugua saratani ya matiti mwanzo na kutibiwa, pia huchochea kuugua tena kama tatizo halikuondoka kikamilifu.
• uzito mkubwa au Unene sana ( kibonge) hupelekea mwanamke kua hatarini kupata saratani hii
• Umri (uzee), mwanamke mwenye umri mkubwa (miaka zaidi ya 50) hua kwenye mazingira hatarishi kupata saratani hili.77% ya wanawake wanaogundulika kua nahii aina ya saratani wanakua kwenye umri wa zaidi ya miaka 50.( www.webmd.com
• Utumiaji au uraji wa vyakula vyenye kemikali nyingi.
• kuanza hedhi mapema kabla ya miaka 12,
• Kuwa na magonjwa mengnine kama vile kisukari (diabetics mellitus)
• Kutokuzaa au kuchelewa kuzaa kwenye umri zaidi ya miaka 35
NAMNA YA KUJIKINGA (PREVENTION) NA SARATANI YA MATITI.
Njia kuu ya kuweza kupunguza nafasi (risk) ya kupata saratani ya matiti ni kubadiri baadhi ya mifumo yetu ya maisha (life style changes).
• Kufanya mazoezi ya mwili (physical exercise) hii itawezesha kuimarisha mwili na kuweka sawa uzito wako.
• Kupunguza unywaji wa pombe
• Kunyonyesha mtoto kwa mwaka mzima au zaidi pia kunapunguza nafasi(chanace) ya kupata tatizo hili.
• Kuijua historia ya familia yako vizuri kuhusiana na saratani hii ya matiti na kufananya uchunguzi wa kitaalamu wa matiti
• Kuacha uvutaji wa sigara
• Kutokutumia madawa yenye muunganiko wa estrogen na progesterone katika umri mkubwa ( miaka zaidi ya 40). Kama zitatumika basi itabidi kupata maelekezo maalumu kutoka kwa daktari.
TIBA YA SARATANI YA MATITI
Tiba inategemea na hatua au ukubwa wa tatizo ulipofikia ( stages of breast cancer). Aina ya tiba ni madawa mbali mbali ikiwemo chemotherapy, tiba ya mionzi (radiotherapy) na upasuaji (surgery) hii hupelekea kukatwa kwa sehemu ya titi au titi lote liliroathiriwa na saratani.
JINSI AMBAVYO MWANAMKE ANAWEZA KUJICHUNGUZA MATATI MWENYEWE.
Fuata hatua hizi:-
1. Jitazame kwenye kioo, mikono yako shika kiunoni. Chunguza vitu hivi.
• Matiti yana umbo,rangi na size ya kawaida?
• Angalia kama chuchu zinatoa uchafu wowote (e.g damu/usaha)
• Chuchu zimebonyea au zimepinduka
• Uvimbe kwenye matiti/titi.
2. Nyanyua mikono yako juu na ishikanishe, kisha jiangalie kwenye kioo.
3. Angalia kama kuna kimiminika (fluids) kinachotoka kwenye chuchu za matiti inaweza kua maji maji,damu, au usaha wa njano).
4. Lala chali kisha tumia mkono wako wa kushoto kubonyeza titi/ziwa la upande wa kulia (tumia sehemu ya mbele ya vidole vitatu vya kati). Anza katikati (kwenye chuchu) kisha zunguka titi zima taratibu kujua kama kuna uvimbe wowote au hali isio ya kawaida kwenye titi. Hivyo hivyo kwenye ziwa la kushoto utatumia mkono wako wa kulia.
NB: Kama utaona au kuhisi zile dalili zote tulizo jadili hapo mwanzo hii itakupa ishara kwamba itakubidi uende hospitali mapema ili kwenda kufanya vipimo( mammography) zaidi kujua tatizo. unaweza kujifunza zaidi juu ya hizi hatua za kujichunguza kupitia mtandao wa you tube ( breast self-exam)
HITIMISHO
Kuna madhara mengiyatokanayo na saratani ya matiti lakini kubwa zaidi ni ongezeko la vifo kua kubwa mwaka hadi mwaka. Hivyo kuna haja ya kuweka juhudi za kupunguza vifo hivi. Upimaji wa saratani hii mapema itasaidia kuweza kupata tiba mapema kabla ya saratani hii haija sambaa na kuathiri sehemu zingine za mwili na kufanya ugumu katika kuitibu.
Hivyo nitoe rai kwa wanawake, njia nzuri ni kujenga mwenendo wa kujichunguza kama nilivoelekeza hapo juu, pia kwenda kufanya screening hospitali ni jambo ambalo litasaidia kuepusha madhara haya pia kurekebisha mifumo yetu mi baya ya maisha kama unywaji wa pombe uvutaji wa sigara na zingine nyingi kama tulivojadili ni mwanzo ni njia bora ya kupunguza nafasi ya kupata saratani ya matiti.

-ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI-
BY ROMANUS MAPUNDA
BSCN
AFISA MUUGUZI
TEL: 0768403171
EMAIL: romanusmapunda5@gmail.com
Comments