Mambo niliyojifunza katika kitabu cha THE COMPOUND EFFECT cha mwandishi DARREN HARDY.

Habari ndugu msomaji wa makala hii!
karibu tuendelee kujifunza ili kuweza kwenda sawa na maish.a ya sasa yasiokwisha changamoto.
As long as you live,keep learning how to live-Lucius Annaeus Senneca.Mwanafalsafa huyu anatuambia"kwakuwa tunaishi,basi hatuna budi kujifunza namna ya kuishi"

Maisha uliyonayo sasa ni matokeo ya mambo mbalimbali madogo madogo uliyoyafanya huko nyuma,maisha  yoyote yale uliyo nayo kwa sasa,ikiwa ni mazuri  au mbaya,bas jua ni matokeo.


Twende moja kwa moja  rafiki tukaangazie yale niliyojifunza kwenye kitabu tajwa hapo juu;
  1.  Hatua ndogo na makini unazochukua katika maisha yako zinakupelekea katika mafanikio makubwa.Ni ukweli usiopingika kuwa mafanikio ni matokeo,sasa ili upate matokeo mazuri kuna mambo mengi unayotakiwa kuyafanya ili uweze kupata matokeo hayo,na mambo hayo wala si makubwa sana ,bali yanafanywa kwa muda mrefu mno mpaka yanakuwa utamaduni au tabia na mwisho huleta matokeo makubwa.
  2.  Kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa kunalipa sana.Binadamu tunapenda matokeo ya papo kwa hapo,yani nipe nikupe,ufanye kazi halafu  baada ya kazi ulipwe mara moja.sasa mafakio hayako hivyo,bali yanakutaka ufanye kazi kwa bidii sana tena muda mrefu bila kukata tama ndipo utakapoona matunda mazuri yakile unachofanya.
  3.  Kila chaguo unalofanya katika maisha yako basi lina athiri moja kwa moja matokeo au mafanikio yako makubwa.Hivyo chagua kilicho bora kwako.
  4.  Mfulilizo wa hatua ndogo ndogo mbaya unazochukua zinakupelekea katika katika maangamizi na majuto makubwa.kama ilivyo kwamba mafanikio ni matokeo,basin a majuto pia ni matokeo.mkusanyiko wa makosa yako mengi katika Nyanja tofauti za maisha yako ndio huleta majuto.
  5.   Jitoe kwa asilimia mia moja bila kutaraji kupata kutoka kwa wengine,wapende wengine kwa asilimia mia moja bila kujali wao wanakupenda kwa kiwango gani au labda  hawakupendi kabisa.
  6.  Chukua jukumu la maisha yako kwa asilimia mia moja,usitegemee mcahngo kutoka kwa mwingine au  yeyote isipokuwa kutoka kwako wewe mwenyewe.Usiilaumu serikali kwa kutokuajiri,hakika serikali haiwajibiki katika kufikia ndoto zako,na hata kama  inawajibika,basi sikwakukupa ajira bali nikwa namna nyingine ambayo huwenda imeshatekeleza.Pia baba yako ama ndugu yako yeyote hawajibiki katika kufikia malengo uliyojiwekea isipokuwa wewe mwenyewe.
  7. Tofauti kati yakuwa  tajiri au kuwa na furaha na kutokuwa na furaha ni hatua au maamuzi uliyoyafanya katika kipindi Fulani cha maisha yako.Na si kitu kingine
  8. Kila mtu ana nafasi ya kuwa na bahati,kama unaishi katika jamii iliyo huru tayari una bahati.bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi.

KANUNI ya kutengeneza bahati

Maandalizi(Ukuaji binafsi)+Mtazamo+Nafasi/fursa+hatua(fanya jambo)=BAHATI.

   9 Bahati zinatuzunguka kila tulipo,ila huwez kuona kile ambacho hujakitafuta,na huwez kutafuta  
    kile ambacho huamini uwepo wake.Pamoja na kwamba bahati zinatuzunguka,ni lazima uitafute ndipo utaiona.na ili utafute kitu lazima uamini kwamba kipo.
        10  “The day you graduate from childhood to adult hood is the day you take full responsibility of your life”Jim Rohn“Siku ambayo unahitimu kutoka hali ya utoto kuingia hali ya utu uzima ndio siku ambayo unabeba mustakabali  mzima wa maisha yako.
11 Chukua hatua sahihi kila siku,kila wiki na kwa miaka,na utashuhudia namna utavyokuwa kiuchumi.kama tulivyoona kuwa matokeo makubwa huletwa na hatua ndogo ndogo ambazo umekuwa unazichukua na kuzifanya kama tabia.

   12 Wekeza asilimia kumi ya kipato chako au kila kinachopita katika mikono yako.hapa sio lazima 
      uwe umeajiriwa nakupokea kila mwisho wa mwezi,hapana.kinachotakiwa nikuhakikisha         

       kila fedha unayoipata labda nifaida katika biashra zako,au malipo yako ya kila siku katika                   kileunachofanya

13     Jambo la msingi nikuanza sasa.usisubiri mpaka uwe tayari ndio uanze,kwani hakuna siku     
       utakuwa tayari kuanza bali kila siku utajiona bado hujawa tayari au kuna mapungufu yanakuzuia.
14 “We are what we repeatedly do”Aristote.tulivyo ni matokeo ya yale tunayofanya mara kwa     
      mara.Sasa ili uwe bora hakikisha unachukua hatua sahihi mara kwa mara.

15 Watu wanaendeshwa na tabia zao bila hata kujua zinawapeleka wapi.tabia tulizojijengea ndio 
   zimekuwa muongozo wetu bila hata ya kujua ni wapi zinakotupeleleka.yapeleke maisha yako     
   katika muelekeo unaotaka.


16   kuwa na viatu vizuri kwa ajili ya mbio za marathon,haitoshi kuwa sababu ya kwamba tuko tayari kwa kuanza mashindano.


17   Haitoshi tu kuchagua kuwa na mafanikio,

18 Unajua ni kipi kinachokuzui kurudi nyuma na kutumbukia katika tabia mbaya ulizokuwa nazo?kuna tabia ambazo uligundua nikikwazo kwako katika kufikia hatua ulizojiwekea malengo nakuamua kuzipiga vita.basi unatakiwa ujue kipi kinakuzuia usirudie tabia izo.

19 Usikazanie mafanikio peke yake bali kutosheka kunakufanya uwe na furaha zaid katika maisha yako.kutosheka na kile ulichonacho kutakufanya uwe na furaha na uyafurahie maisha.kutosheka haina maana usiendelee kutafuta bali kushukuru na kuendelea kuweka juhudi.

20 Mafanikio makubwa hayakuhakikishii kuwa na furaha zaid.furaha inatakiwa itoke ndani yetu na isitegemee vitu vya nje.usitarajie ufanikiwe kwanza ndo uwe na furaha,bali tengeneza furaha kwanza ndio mafanikio yafuate,

21 Maadui zetu wanatupa sababu ya kusimama na kusonga mbele kwa hamasa kubwa.usiogope watu wanaokupinga au kukuchukia katika lile unalofanya,kwani wanakufanya uzidi kuwa nasababu za kufanikiwa

22 Unapoilekeza akili yako katika kile unachokitafuta basi utakiona.hakika dunia ina kila kitu unachohitji,bali ili ukipate lazima uweke juhudi kubwa katika kukipata.

Kanuni  tano za kufuata ili uweze kuondoa tabia mbaya ulizonazo.
ü  Vitambue vichocheo vyako.
Tambua vichocheo vinavyokusukuma katika tabia hiyo mbaya,mfano,mara nyingi unakunywa pombe unapokuwa na watu wa aina Fulani?
ü  Safisha nyumba
Maana yangu hapa ni hii,kama unataka kuacha pombe basi ondoa chupa zote za pombe na vitu vyote unavyotumia wakati wakunywa pombe ndani ya nyumba yako na eneo lako la kazi.kama unataka kuachana na tabia mbaya ya matumizi ya hovyo ya pesa,basi tumia jioni yako katika mambo mengine ya msingi na futa ofa zote unazopokea za kukuomba kujumuika katika maeneo ya starehe.
ü  Badilisha.
Angalia tabia zako zote mbaya,je unaweza kuzibadilisha kwa kitu kingine chenye faida?mfano pale unajiskia kuvuta sigara tafuta kitu kizuri cha kutafuna kwa muda huo ambacho hakina madhara kwa afya yako.


ü  Rahisisha
Baadhi ya tabia zako mbaya umezijenga kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi kuziondoa mara moja,basi usikazane kuziondoa mara moja bali jipe muda.
ü  Ruka.
Badili tabia zako zote mbaya kwa wakati mmoja.

23.      Hutaweza kamwe kubadili maisha yako mpaka ubadili yale unayoyafanya kila siku.kama tulivyokwisha ona kuwa maisha ni matokeo ya hatua unazochukua kila siku,kwaiyo ili ubadli maisha yako lazima ubadili yale unayofanya kila siku.kwani siri ya mafanikio yako iko ndani ya maisha yako ya kila siku.

Kanuni sita zakukusaidia kujijengea tabia nzuri.
a.       Jiweke kimafanikio.
Ondoa au jiweke mbali kabisa na vile vitu ambavyo vinaweza kuwa kikwazo katika safari yako ya mafanikio.na jijengee zile tabia ambazo waliofanikiwa katika jambo ilo  wanazo.
b.      Fikiria sana katika kuongeza na si kupunguza
Mara nyingi wekeza zaidi fikra zako katika kile unachotaka kuongeza na sikile unachotaka kuondoa
c.       Iambie jamii kwamba umebadilika,
unapojua kuwa kuna watu wanakufuatilia mwenendo wako,ni vigumu kurudi kwenye tabia mbaya ambayo ulikuwa nayo na kuwaambia familia,rafiki kuwa umeshaiacha.mfano,kama ulikuwa unavuta sigara,kisha ukawaambia rafiki na ndugu kuwa umeacha kuvuta sigara,basi itakuwa rahisi wewe kuacha kuvuta sigar kwakuwa unajua nikivuta kuna watu wataniona.
d.      Kuwa na rafiki mwenye ndoto kama yakwako,
kuwa na rafiki ambaye atakuwa anakuhamasisha nakukumbusha katika utaratibu mliojiwekea.mfano rafiki ambaye mmepanga mkutane kila siku muda Fulani kwa ajili ya mazoezi.

e.       Fanya mashindano,
kawaida unapojua kuwa uko kwenye mashindano,basi unaweka juhudi ili uweze kuibuka mshindi.ni aina gani ya mashindano unaweza ukafanya na marafiki zako?
f.       Jipongeze,
sasa ni muda wa kujipongeza kwa kufurahia matunda ya ushindi wako.unaweza fanya hivyo kwa namna mbalimbali kama kusoma kitabu kwa ajili ya kujifurahisha au kwenda kutembea

24       Kufanya mambo kwa Kawaida ni rahisi,kufanya mambo katika ubora wa hali ya juu ndicho kitakachokutenganisha na kundi kubwa la watu.binadam hatupendi sana kuwa peke yetu au kuwa tofauti na wengine,hii inatupelekea kufanya vitu kama wengine wanavyofanya na mwisho kupata matokeo yakawaida kabisa,ni pale tu utakapofanya katika ubora ndipo utakapo jitofautisha na kundi kubwa la watu.”The ultimate measure of man is not where he stand in moment of comfort and convenience,but where he stands at time of challenges”Martin luther
25      Jipe muda katika kubadili tabia zako mbaya ambazo umezijenga na kuziishi kwa muda mrefu.tabia hizi unatakiwa kuzibadili taratibu taratibu kwa kuwa zimeshakita mizizi katika maisha yako.
26      Kufikia malengo mapya uliyojiwekea na kutengeneza tabia mpya ni muhimu kuwa na mfumo utakaokusaidia kuyatimiza hayo.binadam kawaida hatupendi sana kubadilika,sasa ili usirudi kwenye mzoea yako ni lazima kuwe na namna yakukusaidia katika hilo.

27     Fikiria mambo yote ambayo unapaswa kushukuru kwayo.kuna wakati huwenda ukahisi maisha yako hayana maana,nikwasababu hujakaa chini na kutafakari zile neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu amekupa.na hii nikwasabab umeelekeza sana fikra zako katika uliyokosa na si yale uliyonayo.
28      Namna ya kupata kutoka kwa wengine ni wewe kutoa kwanza.ili upate upendo kutoka kwa wengine waonyeshe kwanza waonyeshe kwanza wewe upendo.
29      Akili huwa inaendelea kuchanganua taarifa za mwisho ilizopokea kabla ya kulala.hivyo ni muhimu kuilisha akili yako taarifa za msingi na chanya kabla ya kulala.
30      Unashinda pale unapochukua hatua sahihi kila siku,ila unajiweka katika hatua ya kushindwa pale  unapohitaji matokeo ya haraka sana.

     31  Kila mtu anaathiriwa na vitu vitatu.
ü  Unachopokea,kipi unaweka katika kichwa chako.
ü  Unaofungamana nao,wale ambao muda wako mwingi unautumia ukiwa nao.
ü  Mazingira,mazingira yanayokuzuka.

32      Ubongo wako haujatengenezwa kwa ajilinya kukupa furaha.upo kwa ajili ya kuratibu mambo mbalimbali yakukuwezesha kuishi,kwani ubongo ukifa na wewe unakufa.
33      Kichwa chako ni kama glass iliyo tupu,inapokea chochote utakachoweka.kwa maana hiyo ni muhimu kuweka yale yenye kukunufaisha na yenye kukujenga kuwa mtu chanya katika maisha yako.
34.      Vyombo vya habari mara nyingi hukupa taarifa za kusikitisha na kusisimua ili kukutoa kwenye hali yako ya utulivu na mazingatio.
35      Huwezi amabatana na watu ambao ni hasi mara lkwa mara halafu ukategemea kuwa chanya.
36      Kile unachokivumilia katika maisha ndicho unachokipata,kama unavumilia kulipwa mshahara mdogo na kufanya kazi nyingi,hilo ndilo litakaloendelea kwako.
37      Hamasa bila yakuchukua hatua ni sawa na kujidanganya mwenyewe.
38      Wazo lisilofanyiwa kazi limekwishapotea.

Hayo ndio niliyojifunza rafiki katika kitabu hiki.hakika yapo mengi mno ya kujifunza,nakushauri utafute kitabu hiki ili uweze kujifunza zaidi.

Nikutakie safari njema ya mafanikio

Rafiki yako Elishad Bashiru.





Comments

Popular posts from this blog

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

FIKRA PEVU.

SARATANI YA MATITI