TATIZO SIO KIFO, TATIZO NI KILE KINACHOKUFA NDAN YETU TUNGALI HAI.

Habar ndugu msomaj wa makala hii!,karibu tuendelee kujifunza ili kuweza kwenda Sawa na Maisha yasasa yasiokwisha changamoto.
Binadam tofaut na viumbe wengine, kuna uweze mkubwa Sana uko ndan yetu.Uthibitisho wa hilo upo hasa kwenye Mazingira yanayotuzunguka, unapojaribu kutazama Vitu Kwa jicho la fikra, Utagundua Vitu vya ajabu Sana binadam kafanya.vitu hivyo vimeongeza thaman kubwa katika Dunia na Maisha yamekuwa bora sana siku hadi siku.Sasa hivi Unaweza Amka asubuh ukamsalimia mama yako kijijini au ndgu yako ambaye Yuko Marekani ilihali uko bado kitandan Kwa njia ya simu tu either call, Whatsup au hata SMS yakawaida. Kwa kutazama Kawaida Unaweza ona hili ni jambo la Kawaida tu kwakuwa umeshalizoea, ila Kwa Hakika ni kazi kubwa Sana imefanywa mpaka wewe unafurahia Maisha ivyo.watu wamekesha, wamelala njaa mpaka wakagundua simu Kama njia ya mawasiliano. Ukitembea mjini utaona majengo marefu kupita Kias huwez amini kuwa bi/dam Ndo kajenga. Ndege zinatembea angani, meli zenye mizigo ya Tani nyingi sana zinaelea kwenye maji,ni fikra Kias gan zimetumika kugundua Haya? Je Kama kila Mtu angepumzika kwake na mke wake Haya yangetokea Kweli? Bila Shaka Hapana yasingetokea.
Kwanini nimesema hayo yote rafiki yangu? Bila Shaka unajiuliza Swali hili.
Lengo langu nikutaka kukujuza kuwa hata wewe hapo ulipo,ukiwa umesoma au hujasoma kabisa,ukiwa mke au mume, Kwa hali yeyote uliyo nayo, ilihali ni binadam, bas kuna uwezo mkubwa Sana ndan yako Muumba wetu amekuwekea ili uweze kutoa mchango wako kwenye kuongeza thaman kwenye maisha. Kukaa nao huo uwezo bila kuutumia na ukafa nao ni hasara kubwa kuliko hata Hicho kifo chenyewe.Sio lazima Nawewe ugundue simu au gari au meli, hapana.
Vipo Vitu vingi Sana ndan yako Unaweza fanya. Japo hata kufundisha au kushirikisha watu watu kile unachofaham nao nimchango mkubwa kuliko ungekaa nacho mwenyewe.
Kinachotuzuia tusiweze kugundua kipi kipo ndani yetu ni kelele za nje zinazotuzunguka na kutufanya tukose japo dk 5 tukiwa wenyewe, kelele za mitandao ya kijamii, TV, magazeti,kubeti nk, Kuna tuweka busy Kias cha kukosa hata muda wa kukaa tukiwa wenyewe na akili ikiwa huru.
Hivyo rafik, kaa utafakar, je unatoa mchango gani kwenye maisha? Maana unao Usiseme huna.
Pata muda wakukaa mwenyewe Katka Mazingira tulivu iache akili yako iwe huru, utayaona Mengi sana yakipita katika akili yako, usiyapuuze bali yafanyie kazi. Mengine utahisi hayawezekani unajidanganya, ila ukweli nikwamba, Kama umeweza kulifikiria basi linawezekana.
Ukawe na sku njema kabisa yenye mafanikio tele
elishad bashir
Amka na Uishi.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

FIKRA PEVU.

SARATANI YA MATITI