ISHUKURU SANA JANA YAKO
"Use the lessons you have learned from your past to rise to a whole new level of awareness and enlightenments"Robin Sharma.
Habari rafiki!kwanza kabisa hatuna budi kumshukuru Yule aliyetuwezesha kuiona siku hii mpya ambaye ni Mwenyez Mungu Muumba mbingu na ardhi.Hatuna budi pia kuitumia siku hii kuongeza thaman katika Maisha yetu,kwani ni wengi walitamani wawepo ila hawapo.
Karibu sana rafiki.hakika Jana yetu imetawaliwa na mambo Mengi yakiwemo mabonde na milima, makosa na Maudhi pamoja na usaliti mbali mbali lakini yalishapita na Leo tuko katika wakati Wa sasa.Jana yetu ina nafasi kubwa ya kujenga au kuharibu maisha yetu ya sasa.Pale utakapoanza kujilaumu Kwa makosa ambayo uliyafanya na kukupa matokeo mabaya na kukupa wakati mgumu,pale utakapoanza kuwalaumu watu Kwa Yale waliokufanyia mabaya na kujipa sababu kuwa wao wamekuharibia maisha,basi umeamua kupoteze nguvu na muda wako wa sasa kwenye wakati uliopita.Na huo ni uamuzi mbaya Sana katika Maisha yako.Uamuzi sahihi ni pale utakapoamua kujisamehe wewe mwenyewe kwa Yale makosa uliyofanya na kuamua kuyatumia kama somo ili Leo usiyarudie na kuweza kupiga hatua katika Maisha yako.
Uamuzi sahihi ni pale utakapoamua kuwasamehe wale waliokuingiza katika wakati mgumu kwa mambo mbali mbali waliokufanyia ili kuwa huru,na kujifunza kwa Yale waliokufanyia.kama uliwaamini katika biashara, mahusiano,undugu na mambo Mengi kisha wakaenda kinyume, basi utajifunza Leo kutokumuamini mtu Kwa kiwango ambacho uliwaamini wao ili yasitokee tena.kwa namna hiyo Hakika hutailaumu Jana yako, bali utaishukuru Kwa kuwa inakufanya Leo unaishi maisha katika ukamilifu wake.kwani maisha yako, yako mikononi mwako uamuzi ni wako kuyajenga au kuyabomoa, Jim Rohin anatuambia "The day you graduate from childhood to adulthood is the day you take full responsibility for your life "tafsir isiyo rasmi anamaanisha "siku unayobadilika kutoka hali ya utoto na kuingia Hali ya Utu uzima ndio siku unayobeba jukumu zima la maisha yako " kwahiyo kuwalaumu watu nakuwalalamikia rafiki nikupoteza muda wako na Maisha yako. Kibaya zaidi wao wanaendelea na maisha yao na hawana Habari juu ya lolote unalopitia.
Nikutakie kila la kher katika siku yako hii.
@elishad bashiru.
Irshady12@gmail.com.
Comments