FIKRA PEVU.
Usikubali Maisha yako yategemee Vitu hivi:- 1.Pesa. Mtu maskini kuliko wote duniani ni Yule ambaye alicho nacho katika Maisha yake ni pesa tu.niukweli uliowazi kuwa pesa inasaidia upate mahitaji yako ya msingi, uweze kuwasaidia watu wako, uweze kuishi Maisha unayotaka.lakini kama pesa itakuwa ndio sabab yako kuu ya kuishi, basi umechagua Maisha mabaya. Tafuta pesa na miliki kiasi unachohitajii, ila usiache kutengeneza maeneo mengine ya Maisha yako. >Usisahau kuwa bora katika mahusiano yako na watu wengine, >Usitegemee pesa iwe chanzo cha furaha kwako, jitahid kutengeneza furaha kutoka ndan yako. 2.Mahusiano. "The worst loneliness is not to be comfortable with yourself"Mark Twain. Ni kitu kibaya sana kama huwez kuwa na furaha kwakuwa mwenyewe katika Maisha. Furaha yako itakapotegemea Uwepo Wa mtu fulani,ilihali sote tunajua kuwa katika yaliyo nje ya uwezo wetu ni maamuz ya watu wengine,basi umechagua Maisha mabaya kuishi....