Posts

Showing posts from June 17, 2018

Tafakuri ya Maisha.

Kuna wakati katika Maisha unaweza hisi kwamba wewe ndio mwenye matatizo makubwa kuliko watu wote duniani.mpaka unafikia hatua yakujiuliza maswali magumu kwamba Kwanini wewe tu siku zote? Mbona matatizo hayaishi likitoka hili linakuja hili? Nikuambie rafiki yangu,wala huna matatizo makubwa kiasi hicho,tatizo letu kubwa ni kwamba tunaangalia zaidi matatizo yetu kuliko Neema tulizopewa. Na hii nikwasababu tunahisi labda tunastahili zaidi kuwa nazo ndio maana hatuzipi umuhimu wake. Labda umetafuta ajira Kwa muda mrefu bila mafanikio, hilo bado si tatizo kubwa kwako,hivi Unajua kuna Mtu hana miguu Wala mikono lakini bado anafurahia Maisha yake! Kwakuwa anaaamini ana sababu nyingi zakufurahi kuliko kuhuzunika. Wakati wewe unafikiri una matatizo makubwa kwakuwa unaumwa wiki ya Pili sasa. Kuna mwingine kalala kitandani mwaka mzima sasa na hajui mustakabali Wa afya yake. Kuna mwingine Kaambiwa atatumia dawa Maisha yake yote kutokana na maradhi yakudumu aliyo nayo. Kama una miguu na mikono ...

MAISHA

Kuna wakati katika Maisha unapitia mambo  magumu sana, na kila ukijaribu kuondokana na hali hiyo bado hupati majibu sahihi. Nikuambie rafiki, huo ndio wakati unatakiwa kuishi hali hiyo Kwa MUDA!huwa tunasahau kuwa MUDA nao ni tiba ya matatizo yetu.Yape matatizo yako MUDA. kama vile unavyoweza kuipenda nyumba ilihali imefungwa na hujui kilichopo ndani, basi yapende matatizo yako uliyoshindwa kuyatatua. Kuna watu wanapenda nyimbo japo zimeimbwa Kwa Lugha wasioifahamu,kwanini usiipende Hali uliyonayo Kwa MUDa? Kumbuka kila Hali unayopitia Mungu anamakusudi juu yako,huwenda hata matatizo yako yakiondoka sasa hutaweza kuyafurahia Maisha Au hutaweza kuishi katika Hali hiyo tulivu yakukosa changamoto. Nikutakie siku mpya yakuyaendea mafanikio rafiki yangu. Elishad bashir Irshady12@gmail.com. Karibu tujifunze zaidi kwenye amkanauishi.blogspot.com.