MAISHA
Kuna wakati katika Maisha unapitia mambo magumu sana, na kila ukijaribu kuondokana na hali hiyo bado hupati majibu sahihi.
Nikuambie rafiki, huo ndio wakati unatakiwa kuishi hali hiyo Kwa MUDA!huwa tunasahau kuwa MUDA nao ni tiba ya matatizo yetu.Yape matatizo yako MUDA.
kama vile unavyoweza kuipenda nyumba ilihali imefungwa na hujui kilichopo ndani, basi yapende matatizo yako uliyoshindwa kuyatatua.
Kuna watu wanapenda nyimbo japo zimeimbwa Kwa Lugha wasioifahamu,kwanini usiipende Hali uliyonayo Kwa MUDa?
Kumbuka kila Hali unayopitia Mungu anamakusudi juu yako,huwenda hata matatizo yako yakiondoka sasa hutaweza kuyafurahia Maisha Au hutaweza kuishi katika Hali hiyo tulivu yakukosa changamoto.
Nikutakie siku mpya yakuyaendea mafanikio rafiki yangu.
Elishad bashir
Irshady12@gmail.com.
Karibu tujifunze zaidi kwenye
amkanauishi.blogspot.com.
Comments