Tafakuri ya Maisha.

Kuna wakati katika Maisha unaweza hisi kwamba wewe ndio mwenye matatizo makubwa kuliko watu wote duniani.mpaka unafikia hatua yakujiuliza maswali magumu kwamba Kwanini wewe tu siku zote?
Mbona matatizo hayaishi likitoka hili linakuja hili?

Nikuambie rafiki yangu,wala huna matatizo makubwa kiasi hicho,tatizo letu kubwa ni kwamba tunaangalia zaidi matatizo yetu kuliko Neema tulizopewa. Na hii nikwasababu tunahisi labda tunastahili zaidi kuwa nazo ndio maana hatuzipi umuhimu wake.

Labda umetafuta ajira Kwa muda mrefu bila mafanikio, hilo bado si tatizo kubwa kwako,hivi Unajua kuna Mtu hana miguu Wala mikono lakini bado anafurahia Maisha yake! Kwakuwa anaaamini ana sababu nyingi zakufurahi kuliko kuhuzunika.

Wakati wewe unafikiri una matatizo makubwa kwakuwa unaumwa wiki ya Pili sasa. Kuna mwingine kalala kitandani mwaka mzima sasa na hajui mustakabali Wa afya yake. Kuna mwingine Kaambiwa atatumia dawa Maisha yake yote kutokana na maradhi yakudumu aliyo nayo.
Kama una miguu na mikono yako, macho yako yote na afya yako imara kabisa, bado unahisi kuna kitu umekosa mpaka usimshukuru Muumba wako na kufurahia maisha?

Rafiki, naamini umejifunza kitu kwa hayo machache.
Nikutakie siku njema katika kwenda kutatua matatizo uliyonayo.

Elishad bashir
Irshady12@gmail.com.

Comments

Popular posts from this blog

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

FIKRA PEVU.

SARATANI YA MATITI