Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.
Kitu ambacho b,dam anapigania sana katika Maisha yake ni kuwa na Maisha yaliyo nafuraha.kila mtu Anapenda kuwa na furaha katika Maisha yake. Tunatafuta kazi, tunatafuta watoto na tunafanya mengi ila tukiamini yatatimiza hitajio la moyo wetu nakutuletea furaha.Baada yakujua kwamba tunahitaji furaha, shida inakuja kwamba tunaipataje iyo furaha ya Kweli? Ndipo hapo tunapofanya Vitu mbali mbali tukiamini vitatuletea furaha.
Na ile furaha tunayotarajia mwisho wa sku hatuipati kwakuwa hatufuati ile misingi sahihi ambayo ndio hutupelekea kuwa na furaha katika Maisha yetu.
Ndipo mwandishi Wa kitabu, The book of happiness, by Heather Summers & Anne Watson walivyoamua kutuweka wazi juu ya mambo mbali mbali kuhusu furaha.
Haya Hapa ni machache katika niliyojifunza katika kitabu hiki.
1.Mazingira yanayotuzunguka ni moja ya Vitu ambavyo vinaweza kutupa furaha au kutunyima furaha.
Ni hivi, Kama unaishi kwenye nyumba ambayo huipendi, unaishi maeneo ambayo huyapendi,unafanya kazi ambayo huipendi, unafanya kazi na watu ambao huwapendi na vingine vingi katika Mazingira, vinakuwa na mchango mkubwa katika kukunyima furaha.suluhisho Hapa nikubadili Yale ambayo huyapendi katika vinavyokuzunguka, Kama kazi huipendi iache tafuta nyingine ambayo utaipenda na kuifanya Kwa furaha. Badilisha kila kitu ambacho hukipendi na kinakunyima furaha.Kwani Maisha ni mafupi, kufanya kitu ambacho hukipendi nikupoteza muda wako ambao nikitu cha thaman sana.
Napia katika kuongeza furaha, kipambe chumba chako unacholala kiwe kama peponi. Hii itakupa utulivu pale unapokuwa ndani yake, utapata usingizi mzuri na kukuongezea furaha Sana.
2.Unapokuwa na malengo thabiti katika Maisha yako na ukajua kipi hasa unahitaji kwenye maisha yako, unakuwa na utulivu na utulivu huleta furaha.
3.Dhumuni la maisha ndio huleta maana ya Maisha.kwani kwakuwa na dhumuni kwenye maisha yako, utaweza kujibu maswali mengi juu ya Maisha yako.Na wale wanaokosa dhumuni la nini hasa wanahitaji katika Maisha yao hukosa utulivu na kutojitosheleza na Maisha yao.
4.Furaha huja nakuondoka, na wakati mwingine unapita kwenye kipindi cha furaha Sana kwenye maisha yako kuliko kipindi chochote cha furaha ulichowahi kupitia.Kukosa furaha kunayagubika Maisha yako na hujipenyeza kwenye kila eneo,unapokosa furaha kila eneo la maisha yako linaenda hovyo. Mf biashara, mahusiano na kazi, huathiriwa sana na kukosa furaha Kwa mtu.
4.unapokosa furaha unashindwa kuziona Neema ndogo ndogo katika siku yako ambazo zina mchango mkubwa katika kuifanya siku yako iwe Nzuri, Neema hizo ni Kama kuchomoza Kwa jua, Mualiko Wa Chakula kizuri kutoka Kwa rafiki,au jamaa,napia kupata muda wa kujumuika na rafiki wakaribu.
5.Pale unapojichukulia kama mtu usiye na thamani yeyote, kule kujikubali kwako kunashuka na utajiona kwamba wewe si kitu na chochote unachotaka kufanya unahisi hakitakuwa na maana Wala kuleta utofauti wowote katika Maisha yako na jamii pia.
6.Kuna watu wanafikiri kwamba kwasababu hawajawahi kufanya kitu, basi hawawezi kukifanya. Ukweli nikwamba kila kitu kinawezekana pale utakapojiambia mwenyewe kwamba Naweza na ukafanya.
7.Wakati mwingine unaweza kuwa na maarifa juu ya kitu flani lakini ukakosa ujuzi Wa kukifanya. Unaweza jua wazi kabisa nini chakufanya lakini usijue nivipi utafanya. Unahitajika kujifunza namna ya kubadili maarifa uliyonayo kwenda kwenye ujuzi ili uweze kuendeleza kipaji ulicho nacho.
8.pesa peke yake haziwezi kukupa furaha, ila kukosa pesa kunaweza kukupelekea ukakosa furaha. Pesa haiwez kununua upendo. Lakini yote hayo hayaondoi umuhim wa pesa katika Maisha yetu. Bila Shaka Unajua wazi kuwa kitu pekee unachoweza kupata bure bila malipo ni Pumzi, na hii ni pale unapokuwa mzima huna maradhi, Kwa maana hiyo ili maisha yetu yaende vizuri tunahitaji pesa.
9.Kama silaha pekee uliyonayo ni nyundo, basi kila utakachokiona utahisi ni konokono.
10.unapoandika CV yako, Hakikisha unaonyesha mafanikio yako katika kile unachofanya sasa badala yakuonyesha majukumu yako tu.Hii nikwasababu kujua majukumu yako si jambo kubwa, kubwa ni kuyatekeleza.CV ndio kipimo chako kinachoonyesha yaliyotokea kwenye maisha yako.
11.Saa la furaha,tengeneza saa lako la furaha, ambalo utazingatia na kuweka nguvu zako katika kuwa na furaha.
12.Furaha ni kitu cha thaman ambacho tunapigania kukipata, na Huzuni ni kitu ambacho tunajitahidi kuwa mbali nacho.
Hayo ni mambo 12 Niliyojifunza katika kitabu hiki, yapo Mengi Sana yakujifunza Kwani mwandishi ameeleza mambo Mengi Sana.nikushauri ukitafute kitabu hiki na ukisome ili ujifunze zaidi na zaidi.
Nikutakie kila la kher katika kujifunza na kuboresha Maisha yako rafiki yangu. Kwani Maisha bora na yenye ukamilifu ni haki yako ya msingi kabisa.
Elishad bashiru
Irshady12@gmail.com
amkanauishi.blogspot.com.
Andika Comment yako hapo chini rafiki yangu uniambie nikwamna gani umejifunza katika Haya mambo 12,
Pia SUBSCRIBE apo juu kulia Kwa kujaza taarifa zako ili tuendelee kujifunza zaidi.
Comments