MAMBO NILIYOJIFUNZA KATIKA KITABU CHA BLESSED IN DARK PLACES.BY Joel Osteen.


katika maisha watu huwa kuna wakati wanapitia vipindi vigumu.Katika vipindi vigumu ndio wakati ambao mtu huhisi kwamba dunia haimtaki tena na Mungu pia amemsahau.Pia wakati huu ndio wakati ambao mtu huhisi kwamba yeye ndo basi tena,na hawezi tena kurudi katika maisha yake ya mwanzo.
Ila ukweli hauko hivyo,kwani ni katika vipindi vigumu ndipo hutokea washindi.Watu wengi waliofanikiwa katika jambo fulani,ukifuatilia utakuta kuwa walipitishwa kwanza kwenye wakati mgumu ndio yakapatikana matokeo ambayo wengi tunayaona.Mara nyingi tunaangalia matokeo ndio maana tunahisi fulani ana bahati na wewe huna,lakini nyuma ya bahati kuna mchakato amepitia.

Mwandishi Joel Osteen ameelezea mambo makubwa sana katika kitabu chake cha Blessed in the Dark Places.Haya hapa ni baadhi tu ya mambo niliyojifunza kwenye kitabu hicho kutoka ukurasa wa 1-45.
1.Usilalamike sana unapopitia wakati mgumu kwenye maisha yako,huo wakati mgumu ndio Mungu huutumia kupitisha neema zake kwako.
Kwenye wakati huu kikubwa kinachohitajika ni subira na imani juu ya Mwenyezi Mungu,amini kwamba kipindi hicho ni chenye kupita,na hata kama kisipopita bado unatakiwa uaminifu wako kwake usitetereke.

2. Wakati mgumu ni sehemu tu ya mpango wa kutaka kuibua kile kilichopo ndani yako.
Kila mtu ana kitu ndani yake ambacho Mungu amekiweka,lakini mara nyingi kitu hicho hakiwezi kujionyesha mpaka mtu huyo apitie kipindi kigumu kitakachomuhitaji ajitathimini sana na kutumia akili nyingi navipawa vyake.kama ilivyo mbegu haiwezi kuota mpaka ifukiwe ardhini kwenye giza,joto,maji na kila aina ya karaha.

3. Mungu hualipisha watu kwa yale mabaya waliowafanyia wengine.
Kuna watu wanaweza kukufanyia mabaya na kukusababishia machungu kwenye maisha,lakini Mungu humlipa mtu kwa yale mabaya aliofanyia wengine.waswahili husema “Malipo ni hapa hapa duniani”
4. Changamoto unayopitia inaweza kuonekana kubwa na usioweza kupambana nayo.Ila kumbuka  kwa Mwenyezi Mungu hakuna linaloshindikana.
Haijalishi changamoto unayopitia ina ukubwa gani,ukimuamini Mungu kwa uwezo wake hakuna linaloshindikana.

5.Huwenda kwasasa uko kwenye wakati mgumu shida na taabu zinakuandama,ila kumbuka hicho ni kipindi cha mpito tu,kuna kitu Mungu anafanya juu yako na utakuja kukishuhudia.

6.Usikubali changamoto za maisha zikutoe kwenye lengo  na kukata tamaa katika zile ndoto zako kubwa ulizo nazo,hakika changamoto zipo tu,kwaiyo zenyewe sio tatizo sana,tatizo ni wewe namna unavyozipokea.

7.tabia njema za mafanikio hujengeka kwa mtu pale anapopitia kipindi kigumu na mambo yake hayaeleweki,ila akaendelea kufanya yale yaliyo sahihi na yamuhimu.

8.Mungu huwa hakupitishi kwenye njia nyepesi na yawazi,anakupitisha kwenye njia ngumu inayoambatana na kupoteza vile vyenye thamani kwako,kukataliwa,kuvunjwa moyo,kuachwa na kila aina ya mateso.Na yote hayo ni sehemu ya mipango yake juu yako.

9.wakati mwingine vikwazo na kuvunjwa moyo ni sehemu ya majaribu,Mwenyezi Mungu anataka kujua je utaendelea kumuamini hata kipindi ambcho mambo yako yanaenda hovyo?.

Hayo ndio baadhi ya mambo niliyojifunza mwanzoni kabisa mwa kitabu hiki kizuri kabisa kinachokujengea ujasiri wa kuishi na kufurahia maisha hata kama uko kwenye akati mgumu.Kinakufanya uitue mizigo uliyoibeba na kuikabidhi kwa Mwenyezi Mungu ambaye hashindwi na lolote chini ya jua.

Elishad bashiru


Comments

Popular posts from this blog

Uchambuzi Wa kitabu;MAMBO 12 Niliyojifunza katika kitabu cha THE BOOK OF HAPPINESS.

FIKRA PEVU.

SARATANI YA MATITI