Kitu ambacho b,dam anapigania sana katika Maisha yake ni kuwa na Maisha yaliyo nafuraha.kila mtu Anapenda kuwa na furaha katika Maisha yake. Tunatafuta kazi, tunatafuta watoto na tunafanya mengi ila tukiamini yatatimiza hitajio la moyo wetu nakutuletea furaha.Baada yakujua kwamba tunahitaji furaha, shida inakuja kwamba tunaipataje iyo furaha ya Kweli? Ndipo hapo tunapofanya Vitu mbali mbali tukiamini vitatuletea furaha. Na ile furaha tunayotarajia mwisho wa sku hatuipati kwakuwa hatufuati ile misingi sahihi ambayo ndio hutupelekea kuwa na furaha katika Maisha yetu. Ndipo mwandishi Wa kitabu, The book of happiness, by Heather Summers & Anne Watson walivyoamua kutuweka wazi juu ya mambo mbali mbali kuhusu furaha. Haya Hapa ni machache katika niliyojifunza katika kitabu hiki. 1 .Mazingira yanayotuzunguka ni moja ya Vitu ambavyo vinaweza kutupa furaha au kutunyima furaha. Ni hivi, Kama unaishi kwenye nyumba ambayo huipendi, unaishi maeneo ambayo huyapendi,unafanya kazi ambayo...
Comments